Vidokezo
Beba sweta ama koti
Msimu wa kiangazi wa Hong Kong ina joto jingi sana. Ni jambo la busara kubeba sweta au koti la kuvalia ukiwa jumbani kwani vifaa vya kuvifanya majumba yasiwe na joto sana kwa wakati mwingine huyafanya majumba kuwa baridi mno. Hivyo basi waweza kutahitaji sweta.
Msimu wa kiangazi wa Hong Kong pia huwa na mvua nyingi. Fuata maagizo ya utabiri wa hali wa hewa, ili kujua kama mvua inatarajiwa. Unaweza kuubeba mwavuli ama kabuti za kuzuia mvua; au kuvalia koti lisilolowa maji lililo na kofia.
Beba pasi au kitambulisho rasmi lako kila wakati.
Polisi wa Hong Kong wana haki ya kumsamimisha mtu yeyote na kumuamrisha ajitambulishe, na mara nyingi wao hufanya hivyo, kulingana na mujibu wa sheria. [1]
Ukihitaji kutumia mtandao kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hong Kong (HKG)
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hong Kong ina mtandao usiolipiwa. Ni jambo la busara kuitumia iwapo una haja kabla hujajisajili na maafisa wa uhamiaji. Sababu ni kwamba ukishapita hapo, ni vigumu kuupata mtandao kwani watu wengi huwa wanaitumia.
Hakuna kula wala kunywa katika treni na mabasi
Hairuhusiwi kula au kunywa ukiwa kwenye basi na treni. Waweza kutozwa faini na wlinda usalama au washirika wa stesheni. Abiria wengine pia wanaweza kukutahadhirisha dhidi ya kula au kunywa.
Hakuna uvutaji wa sigara ndani ya nyumba (na wakati mwingine pia nje!)
Hong Kong imepitisha sheria inayozuia uvutaji sigara mahalli mbali mbali kutoka tarehe mosi, Januari 2007. Kuvuta au kuonekana na sigara mahali pasiporuhusiwa kuwa na sigara ni kosa linaloadhibiwa kwa kutozwa faini ya $1,500.[2]
Bali na mahali palipo ndani ya majengo kama mikahawa, ofisi na madukani, uvutaji sigara imepigwa marufuku machuoni (kama vile mahali ambapo kongamano la Wikimania 2013 litakuwa!), mabustani na kwenye vyombo na majumba (kama vile mastesheni) yatumikayo kwa usafiri wa umma. Mikahawa iliyo nje ndio hutumika sana sana na wavuta sigara.
Endesha gari lako upande wa kushoto barabarani
Magari mjini Hong Kong huendeshwa upande wa kushoto wa barabara, wala sio upande wa kulia kama ilivyo Uchina au nchi zingine jirani, kwani ni mfumo unaiga ule wa Uingereza. Kukata kwa kushoto wakati mataa ya trafiki ni nyekundu hairuhusiwi, ili wanaotembea waweze kuvuka barabara bila wasiwasi.
Simama upande wa kulia kwenye ngazi zinazovutwa kwa stima
Ukiwa unatembea kwenye ngazi zinavutwa na stima (escalator, kwa Kiingereza), simama upande wa kulia, kwani upande wa kushoto ni upande wa wale wanaotaka kuendelea kutembea.
Hivyo basi, kila wakati kumbuka kutembelea upande wa kushoto, simama upande wa kulia!
Tahadhari za hali mbaya ya anga
Halmashauri ya hali ya anga ya Hong Kong inazo ilani kadha wa kadha za kutahadhirisha umma dhidi ya hali mbaya ya anga na kuwawezesha watu kufanya mipango ifaayo kulingana na hali ya anga.
Hizi ni baadhi ya ilani zitumikazo haswa katika msimu wa kiangazi.
- Ilani ya mvua nyingi sana
- Ilani ya mvua nyingi iliyo na upepo wa kasi
- Ilani ya joto jingi sana
Tahadhari inapotolewa, kanda nyingi za habari huzichapisha hivyo basi kuwatahadhirisha watu wengi sana.
- Kurasa za mtandao ya halmashauri ya hali ya anga ya Hong Kong iliyo na habari kuhusu hali ya anga.
- Tahadhari itolewayo moja kwa moja kuhusu hali ya anga
Tahadhari za hali ya anga zinapotolewa (kwa mfano , au hali mbaya zaidi) wafanyi biashara na huduma za uchukuzi kama basi na feri hukatiza huduma hadi wakapo tahadhari zitafutiliwa mbali. Ni muhimu kupanga safari wakati kama huu.
Ingawa mvua nyingi, hata zile zinazo kuja na upepo mwingi sana, kwa kawaida hazisababishi uharibufu mkubwa mijini, ukiwa mahali ambapi ni mbali na miji mikuu ni jambo la busara kuwa mwangalifu zaidi. Kukiwa na hali mbaya sana, jisalimishe ndani ya jumba na upige simu nambari 999.